Dakika 45 za Kipindi cha Kwanza zimekamilika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Yanga dhidi ya TP Mazembe.
Ni Wananchi Yanga wanaokwenda kifua mbele wakiwa na uongozi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na wachezaji waliojiunga dirisha dogo la Januari Kennedy Musonda na Mudathir Yahaya aliepachika bao la pili.
Musonda ndie aliekuwa wa kwanza kuwapa Yanga bao la uongozi akimaliza mpira wa adhabu uliopigwa na beki Djuma Shaban kisha Musonda huyo huyo akatoa pasi safi ya goli kwa Mudathir Yahaya.
Mbali na magoli hayo kuna nafasi kadhaa ambazo Yanga wametengeneza lakini kukosa umakini kumewafanya kushindwa kuzibadilisha na kuwa magoli.