Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SGR Mutale hatihati kuikosa Singida Big Stars

Mutale 8Gc.jpeg SGR Mutale hatihati kuikosa Singida Big Stars

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema, winga wao Joshua Mutale 'SGR' alipata majeraha na kwamba kuna asilimia kubwa akaukosa mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars.

Ahmed amesema, nyota huyo waliyemsajili kwenye dirisha kubwa lililopita, aliumia nyama za paja na kwa mujibu wa madaktari, atakaa nje ya uwanja kwa takriban siku nne mpaka tano.

“Kuna asilimia kubwa ya kukosa mchezo dhidi ya Fountaine Gate” maneno ya Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally akizungumzia hali ya nyota Mutale.

Mechi hiyo inatarajia kupigwa Agosti 25, 2024 katika dimba la KMC Mwenge jijini Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live