Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SERENGETI BOYS, UGANDA VITANI LEO

3ee04efdfedef536d8ff75a959d46bfd SERENGETI BOYS, UGANDA VITANI LEO

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imedhamiria kuibuka na ushindi katika mchezo wa fainali wa mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) dhidi ya Uganda utakaochezwa Uwanja wa Umuganda Rubavu Rwanda leo.

Akizungumza na gazeti hili jana, kocha wa timu hiyo, Hababuu Ali alisema wanajua wanakwenda kucheza na timu ambayo haijafungwa ikiwa imefunga mabao tisa bila kurusu kufungwa, lakini nia yao ni kulipa kisasi cha timu ya U20 kuvuliwa ubingwa na kaka zao Uganda.

“Uganda ni timu nzuri haijafungwa lakini pia sisi hatujafungwa. Shauku yetu ni kuchukua ubingwa ili kuwafuta machozi timu ya U20 ambayo ilivuliwa ubingwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mjini Arusha,” alisema Hababuu.

Pia alisema watamkosa mshambuliaji wao hodari Kassim Yahya ambaye ana kadi nyekundu lakini Omar Mvungi atacheza baada ya kukosa mchezo uliopita kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Aidha, alisema kwa vile wameshakata tiketi ya kwenda Morocco mwakani lengo ni kurudi na kombe na kujigamba wanastahili maana wana kikosi kizuri. Tanzania hii ni mara ya mara tatu mfululizo kufuzu na imefika fainali baada ya kuifunga Ethiopia kwa penalti 4-3 baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya 1-1 na Uganda waliifunga Djibouti kwa bao 1-0.

Hata hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na vikosi vyote kuwa na wachezaji wazuri wenye mbinu na ufundi ingawa Uganda wanaweza kufaidika kwa sababu ya kuwa na miili mikubwa.

Kabla ya mechi hiyo, utachezwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Ethiopia na Djibouti kwenye kwenye uwanja huo huo. Mashindano hayo ambayo yanafikia tamati leo yalishirikisha timu sita zilizopangwa kwenye makundi mawili, ambapo Kundi A lilikuwa na Uganda, Kenya na Ethiopia na Kundi B likiwa na wenyeji Rwanda, Tanzania na Djibouti.

Chanzo: habarileo.co.tz