Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SBS vs Yanga Ligi Kuu Mei 4, ASFC Mei 7

Singida Hj SBS vs Yanga Ligi Kuu Mei 4, ASFC Mei 7

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Rasmi Singida Big Stars itacheza dhidi ya Yanga Mei 7 mwaka huu katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sport Federation (ASFC) na Ligi Kuu Bara Mei 4 mwaka huu, michezo yote ikipigwa katika Uwanja wa Liti mkoani Singida.

SBS imepata nafasi kucheza nusu fainali mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mbeya City uliofanyika katika Uwanja wa Liti huku Yanga wakiifunga Geita Gold kwa bao1-0 katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es salaam.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es salaam, SBS ilikubali kichapo cha mabao 4-1.

SBS inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 51,imeshinda michezo 15 na kufungwa mitano huku Yanga ikiongoza ikiwa na pointi 68.

Msemaji wa timu hiyo, Hussein Massanza amesema wamepokea barua asubuhi ya leo ikiwaelekeza kuhusu michezo hiyo.

Amesema wanaanza maandalizi kujiandaa na michezo hiyo na imani yao watafanya vizuri.

Chanzo: Mwanaspoti