Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sébastien Haller na simulizi ya huzuni ya maisha yake

Sebastian Haller Zx Sébastien Haller.

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaitwa Sébastien Romain Teddy Haller (29), mshambuliaji hatari zaidi katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Ivory Coast, amezaliwa Juni 22, 1994 Ufaransa, baba yake ni Raia wa Ufaransa na Mama yake ni Raia wa Ivory Coast.

Nyota huyu wa Borussia Dortmund ya Ujerumani amewahi kulala kitandani kwa muda wa miezi sita akipambana na kansa, wengi wakaamini Historia yake katika Soka imefikia tamati, lakini mambo yakabadilika. Haller akarudi tena Dimbani na sasa ameipeleka fainali Ivory Coast.

Hakucheza mchezo wowote hatua ya Makundi hadi tulipomwona hatua ya 16 Bora dhidi ya Senegal aliingia kutoka benchi. Baada ya uwepo wake ndani ya pitch, Ivory Coast wakaanza kuwa Bora zaidi.

Haller alipiga pasi ya kupenyeza ndani ya box la Senegal ikamkuta Nicolas Pepe ambaye alifanyiwa madhambi na Golikipa wa Edwardo Mendy Frank Kessie akafunga bao la kusawazisha Kwa penati.

Katika mchezo wa Robo fainali dhidi ya Mali aliingia kutoka benchi timu yake ikiwa nyuma ujio wake uliifanya itengeneze mashambulizi ya Nguvu na kupata mabao mawili.

Jana ana ibeba Ivory Coast kutinga fainali katika michuano ya AFCON 2023 na kufuta ule mwiko wa mwenyeji kutofanya vema katika michuano hiii.

Kazi ya Sebastian Haller Kwa sasa ni kuwapa Ubingwa Ivory Coast katika mchezo wa fainali Kwa njia aliyopita Sina shaka na hilo Ivory Coast ni Bingwa wa AFCON 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live