Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rwanda yajipigia Afrika Kusini

Rwanda Afrika Kusini (18).jpeg Rwanda yajipigia Afrika Kusini

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya South Africa licha ya kuwa na mastaa wengi wanaotamba katika Ligi ya Mabingwa Afrika na wanacheza timu kubwa Africa kama Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Kaizer Chief, Orlando Pirates lakini wamekuwa hawafanyi vizuri.

Leo Afrika Kusini imekubali kuchezea kipigo cha bao 2-0 dhidi ya Rwanda ambao sio timu tishio barani Africa katika mchezo wa Kundi C kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 uliopigwa katika Dimba la Huye.

Mabao ya Rwanda maarufu kama Amavubi yote yamefungwa kipindi cha kwanza na Innocent Nshuti dakika ya 12 na Gilbert Mugisha dakika ya 28.

Mashabiki wa timu ya taifa ya Africa kusini wamechukizwa na kipigo cha leo wakisema wachezaji wao hawajitumi kama kwenye klabu zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live