Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu yaanda "Sapraizi" kwa Mkapa

YOUNG SC Kikosi cha Yanga cha msimu wa 2021-2022

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huenda usiku wa leo nchi na hasa katika upande wa michezo ikasimama kwa kujadili kile ambacho kinakwenda kufanywa na Maafande wa Ruvu Shooting kutoka kule Mlandizi Mkoani Pwani ndani ya dimba la Mkapa

Ruvu wanataka kufanya kile ambacho kimeshindwa kufanyika na timu nne zilizocheza na Yanga mpaka sasa, kuifunga timu hiyo ya mitaa ya Jangwani.

Kuelekea kwenye mchezo huo, Kocha msaidizi wa klabu ya Ruvu, Rajab Nakuchema amejinasibu kuwa, Ruvu wazee wa mpapaso ndiyo itakuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga kwa msimu huu wa mwaka 2021-2022.

“Sisi tutakuwa timu ya kwanza kufungua mlango wao. Tunaimani tutakuwa wa kwanza kuifungaYanga msimu huu” Alisema Rajab Nakuchema wakati anazungumza na wanahabari kwenye mahojiano kabla ya mchezo.

Upande mwingine, Kocha na Nahodha wa klabu ya Yanga hawakuweza kutokea kwenye mahojiano hao kwasababu ambazo mpaka sasa hazijatajwa na kufanyiwa changanuzi na bodi ya Ligi.

Mpaka sasa, Yanga imecheza michezo yake 4 na kupata ushindi kwenye michezo yote, ikifunga mabao 6, ikiwa haijaruhusu bao la kufungwa hata moja na kufikisha alama 12 ambazo zinamfanya awe kinara kwenye msimamo wa ligi.

Kwa Upande wa Ruvu Shooting, wenyewe wanashika nafasi ya 8 ikiwa na alama 6. Mchezo mwingine utakaochezzwa leo, ni  Azam FC ambao watawakaribisha waima dhahabu kutoka mkoani Geita, timu ya Geita Gold saa 2:30 usiku, Chamazi 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live