Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting yatinga robo fainali

Mtanda Pic Ruvu Shooting yatinga robo fainali

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ruvu Shooting U-20 imemaliza mchezo ya makundi katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Wilaya Morogoro 2022 kwa kuifunga Save Talent Academy bao 8-0 kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Morogoro.

Vijana hao wa Kocha Frank Msese ni waalikwa katika michuano hiyo na michezo ya makundi imekuwa ikitoa vipigo vikali dhidi ya wapinzani wao na kutinga hatua ya robo fainali.

Akizungumza mjini hapa, Kocha mkuu wa timu ya Save Talent Academy, John Mbwana amesema wapinzani wao wakulikuwa bora dhidi yao na wachofikiria kwa sasa ni kujiandaa na mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya michuano ya vijana U20 kuwa migumu kwao kwa kushindwa kutamba.

Kocha Mbwana amesema ligi ya vijana U-20 kwao ilikuwa ngumu na changamoto kwani wameshindwa kupata matokeo katika michezo mitano ya makundi walioshuka dimbani na jambo hilo linawafanya kurudisha nyuma majeshi kwa lengo la kujipanga kwa mashindano yajayo ya vijana ya U-17.

“Wachezaji wangu wengi ni wageni na wapya kushiriki michuano mikubwa kama hii, kwa upande wetu tumejifunza jambo kutoka kwa wenzetu na sasa tunajipanga kwa michuano yajayo ya U-17, tunasikitika kuwa tumepoteza michezo yote mitano mbele ya wapinzani wetu inatosha tu kusema tumejifunza na mapungufu yetu tunayafanyia kazi.” amesema Mbwana.

Save Talent Academy ilianza kutanguliza mguu wa kushoto katika michezo hiyo kwa kukubali kupoteza mchezo wa kwanza katika kundi lao kwa kuchapwa bao 1-0 na Kilakala Academy kisha ikapokea kipigoc ha bao 5-0 mbele ya Moro Kids kabla ya kufungwa bao 4-2 na Black Viba.

Kocha wa Ruvu Shooting, Frank Msese amesema michezo ya makundi walianza vizuri kwa kupata ushindi wa bao 5-0 mbele ya Chamwino Youth na kumaliza vizuri mchezo wa mwisho hatua hiyo kwa kupata ushindi wa mabao 8-0.

“Tumeingia robo fainali baada ya kufanya vizuri hatua ya makundi ambapo tutakutana na Fountain Gate tunatambua michezo ya makundi kulikuwa na timu dhaifa na imani yetu timu zilizoingia robo zimestahili kufika hatua hiyo ya robo fainali kuwa ni timu nzuri.” amsema Msese.

Msese amesema kati ya michezo mitano ya hatua ya makundi wameshinda michezo minne na kutoa sare mmoja hivyo amewatahadharisha vijana wake kuwa makini dhidi ya Fountain Gate na kutengeneza nafasi nyingine ya mabao ili kupata matokeo ndani ya dakika 90 na kinyume cha hapo anayepoteza maana yake anaaga mashindano hayo na watakuwa hawajatimiza lengo lao.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz