Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting yashtuka, yahamia uwanja wa Ihefu

HIGHLAND ESTATE Ruvu Shooting yashtuka, yahamia uwanja wa Ihefu

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wadau na mashabiki wa soka mkoani Iringa wamesema kutotumia uwanja wa Samora ni sababu inayoipa matokeo mabovu Ruvu Shooting wakidai inakosa sapoti wakiomba irejeshwe haraka.

Ruvu ambayo iliuzwa kwa Lipuli, inatumia uwanja wa Jamhuri, Morogoro na haijawa na mwenendo mzuri ikicheza mechi nne bila kushinda wala kupata sare na kuwa mkiani.

Derick Sanga alisema wao kama wadau na mashabiki walipokea kwa furaha taarifa za kununua timu ya Championship, lakini hawafurahishwi na matokeo iliyonayo timu hiyo hadi sasa.

Alisema kilichowachanganya zaidi ni timu hiyo kutotumia uwanja wa Samora mkoani Iringa au mwingine uliopo karibu na mashabiki badala yake kupelekwa mkoani Morogoro.

“Kule ilipo haina sapoti ya dhati kutoka kwa mashabiki na wadau, mwisho itapoteza ile dhamira ya waliojitolea kununua timu ili wana Iringa tupate burudani, tunataka irejeshwe nyumbani,” alisema Sanga.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Ramadhan Mahanu alisema kwa sasa bado ni ngumu kuirejesha Samora kutokana na uwanja kutokuwa vizuri badala yake wanafikiria kuhamia Highland Estate mkoani Mbeya.

“Mashabiki na wadau wawe na utulivu, bodi ya ligi ilitupa viwanja viwili Jamhuri na Highland Estate Mbarali, hivyo tunaangalia matokeo ya mechi zijazo tuone tunafanyaje,” alisema Mahanu.

Chanzo: Mwanaspoti