Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting yaipapasa Gwambina

Ruvugwambina Data Ruvu Shooting yaipapasa Gwambina

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Saddam SadickMore by this Author Mwanza. Bao la dakika 47 lililofungwa na Frank Ikobela limeiwezesha Ruvu Shooting kuondoka na pointi tatu muhimu ugenini dhidi ya Gwambina, katika mchezo uliopigwa dimba la Gwambina mkoani hapa.Ruvu Shooting ilishuka dimbani ikikumbuka kupoteza mechi yake iliyopita ikiwa nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu, ambapo leo Jumanne imejipoza kwa wapinzani hao kwa kipondo hicho.Licha ya wachezaji wa timu zote kucheza kwa jihadi kusaka ushindi, lakini ishu ya uwanja iliwanyima nafasi kuonesha uwezo wao zaidi kutokana na kujaa maji kufuatia hali ya mvua iliyonyesha kabla ya mchezo huo.Katika dakika 45 za awali, timu hizo licha ya kosa kosa za hapa na pale lakini iliwafanya wapinzani hao kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa ya bila kufungana, japokuwa Maafande walionekana kuwazidi wenyeji haswa suala la fiziki.Kipindi cha pili kiliwapa faida Ruvu Shooting kutokana na kutumia vyema nafasi moja kati ya kadhaa walizopata na kuwafanya kufikisha pointi 31 wakiendelea kubaki kwenye nafasi yao ya tano.Matokeo hayo si rafiki kwa Gwambina ambayo mchezo uliopita walilazimisha sare dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1-1 wakiwa mjini Bukoba, kwani inawafanya kubaki nafasi ya 15 kwa alama zao 20

Chanzo: mwanaspoti.co.tz