Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting yaiadabisha Coastal Union

Ruvu Ruvu.jpeg Kikosi cha Ruvu Shooting

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao pekee la Saadat Mohamed dakika ya 61 limeipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inayofundishwa na kocha mzoefu, Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ inafikisha pointi sita baada ya mechi tatu za mwanzo kufuatia kufungwa 1-0 na Dodoma Jiji FC Jijini Dodoma na kushinda 1-0 dhidi ya Biashara United mjini Musoma na leo ikicheza nyumbani kwa mara ya kwanza msimu huu inang’ara.

Hali si nzuri kwa Wagosi wa Kaya ambao leo wamekamilisha mechi tatu bila ushindi kufuatia sare mbili za nyumbani 1-1 na Azam FC na 0-0 na KMC Uwanja wa Mkwakwani Jijiji Tanga.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbeya Kwanza imelazimishwa sare ya 0-0 na Dodoma Jiji Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mbeya Kwanza inafikisha pointi tano baada ya mechi tatu, ikitoka kushinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ugenini na sare nyingine ya 2-2 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Mbeya City, wakati Dodoma Jiji baada ya kuichapa Ruvu 1-0 nayo ilichapwa 1-0 na Simba nyumbani, Uwanja wa Jamhuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live