Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting wamejipanga kisawa sawa

RUVU SHOOTING Wachezaji wa kikosi cha Ruvu Shooting

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo yamepamba moto ndivyo unavyoweza kusema, wakati wenyeji wa Mlandizi Ruvu Shooting inapokwenda kutuonsesha wapiganaji wake waliopewa dhamana kuhakikisha wanaiweka salama timu hiyo kwa msimu wa 2021/2022.

Ruvu Shooting imejitapa kutangaza wanajeshi wake 25 watakao ingia kambini kujiweka sawa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara, utakaoanza mwezi ujao.

Ruvu walimaliza nafasi ya 11 katika msimu uliomalizika wakiwa na alama 41 wamesema katika wachezaji watakao watambulisha kutakuwa na maingizo mapya nane ili kuimarisha kikosi chao.

Akizungumza ma Mwanaspoti Afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire anasema baada ya klabu yao kukamilisha usajili wa msimu 2021/2022 kinachofuata ni kuwafahamisha Mashabiki nani yupo na nani hayupo ila waliopo wanaweza kutimiza kiu ya mashabiki wa ruvu.

"Suala la usajili kulingana na mahitaji ya kocha umekamilika na tunategemea kesho kutangaza kikosi chetu na lini wataingia kambini rasmi kujianda na msimu", amesema Masau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live