Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting wamechelewa sana kushuka daraja

Ruvu Shootinga Vs Mbeya Ruvu Shooting wamechelewa sana kushuka daraja

Sat, 20 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wale Ruvu Shooting sijui tuwape pole au tuwapongeze baada ya kushuka daraja na sasa hatutawaona kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu ujao ila watapatikana ligi ya Championship.

Unajua kwa nini kijiweni wanajiuliza hivyo? Ni kwa sababu inasikitisha jamaa kushuka daraja lakini ukiangalia kwa hali ilivyokuwa ni kama wamestahili bwana kwenda huko chini.

Sawa ngoja tuanze kuwapa pole kwanza maana ukiikosa Ligi Kuu ya NBC kwa miaka hii ya sasa ni maumivu makubwa.

Kwanza timu yako haitaonekana katika kituo kikubwa cha luninga nchini cha Azam TV ambacho kinadhamini ligi hiyo upande wa haki za matangazo ya luninga lakini kubwa zaidi hutopata kiasi cha Sh 500 milioni ambacho kila timu inakipata kutoka katika udhamini huo emu fikiria.

Kama hauonekani na kituo kikubwa cha luninga kama hicho maana yake wale wadhamini binafsi ambao walikuwa na mpango wa kuja kwako hutowapata tena na utaishia kuendesha timu kwa kutegemea fedha za mifukoni mwa watu, hapo ndipo utaujua vizuri udume wa ligi ya Championship.

Lakini kwa upande mwingine acha tu tuwapongeze kwa kuchelewa kushuka daraja hadi katika raundi ya 28 zikiwa zimebaki raundi mbili tu msimu kumalizika.

Jamaa walitakiwa wahsuke mapema msimu huu na jambo la kushukuru ni kusuasua tu kwa baadhi ya wapinzani wao katika ushindani wa kupigania kubakia ligi kuu.

Kushuka daraja kwa Ruvu Shooting kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na wao wenyewe na sio ushindani mkubwa kutoka timu nyingine.

Kama ilivyo utamaduni wao, nyakati fulani wachezaji muhimu walikiacha kikosi na kwenda katika mafunzo tena wale muhimu jambo lililolipa kazi ngumu benchi la ufundi.

Wakati wa usajili, haikupata wachezaji wa daraja la juu na badala yake ikawachukua wale ambao hawakuwa na uwezo wa kuiongezea thamani timu.

Acha wakajipumzikie katika Ligi ya Championship pengine watarudi wakiwa na moto zaidi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: