Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting waichapa Mbeya City Sokoine

Ruvu Shootinga Vs Mbeya Ruvu Shooting waichapa Mbeya City Sokoine

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Ruvu Shooting katika mchezo huo yamefungwa na Valentino Mashaka dakika ya 30 na Abrahman Mussa dakika ya 81, wakati la Mbeya City limefungwa na Sixtus Sabilo dakika ya 41 kwa penalti.

Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 15, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 27 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 25.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live