Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting waichapa Geita Gold Mabatini

Ruvu Win 2 1 Ruvu imejikusanyia alama tatu baada ya kushinda

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafande wa Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Mabao ya Ruvu Shooting yamefungwa na Hamad Majimengi dakika ya 53 na Elias Maguri dakika ya 87 baada ya Geita Gold kutangulia na bao la Offen Chikola dakika ya 24.

Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya 13, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 31 za mechi 23 sasa nafasi ya tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live