Klabu ya Soka ya Lipuli FC ya Mkoani Iringa inayoshiriki ligi daraja la pili inatarajiwa kurudi ligi daraja la kwanza (Championship) baada ya wadau wa soka wa mkoani Iringa kuinunua klabu ya Ruvu Shooting ya daraja la kwanza katika mpango unaolenga kuibadili jina ili itambulike kama Lipuli FC.
Mchakato huo utaifanya Klabu ya African Wanderers ya mjini Iringa inayoshiriki ligi daraja la nne ngazi ya Wilaya kupanda hadi daraja la pili baada ya kukamilisha mchakato wa kuchukua nafasi ya Lipuli FC.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada amezungumza na wanahabari Agosti 30 na kusema Utaratibu wa kuinunua Ruvu Shooting tayari umekamilika na wakati wowote kuanzia sasa timu hiyo itawasili Mkoani Iringa.
Katika hatua nyingine Ngwada amesema utaratibu wa kubadili jina la klabu hiyo ili ijulikane kama Lipuli FC unaendelea.