Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting ni muujiza tu, hesabu zinagoma

Ruvu SSSS Ruvu Shooting ni muujiza tu, hesabu zinagoma

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya matumaini waliyonayo Ruvu Shooting kubaki Championship lakini hesabu zinaiondoa kwenye ligi hiyo iliyobakiza mechi tano kumalizika.

Timu hiyo iliyowahi kucheza Ligi Kuu kwa misimu tofauti, ilishuka msimu uliopita na haijawa na mwenendo mzuri ikiwa mkiani kwa pointi 11 hadi sasa.

Maafande hao waliokuwa wakimilikiwa na Jeshi la Wananchi kabla ya kupigwa bei Manispaa ya Iringa na katika michezo mitano iliyobaki itacheza miwili nyumbani na mitatu ugenini.

Katika mechi hizo, itaanzia nyumbani dhidi ya Stand United, kisha kucheza mbili ugenini mbele ya Pan African na Cosmopolitan, itarudi nyumbani kukipiga na Transit Camp na kuhitimisha kwa Green Warriors.

Iwapo itashinda mechi zote, itafikisha pointi 26 ambazo zitawaweka kwenye hesabu za mchujo ‘play off’ kuwania kubaki kwenye ligi, lakini vinginevyo itaondoka na maji.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Julio Elieza alikiri ugumu wa ratiba hiyo huku akiahidi mechi hizo hawataki sare wala kupoteza bali pointi tatu.

Alisema anachofanya kwa sasa ni kuwaweka vijana wake fiti kisaikolojia kuhakikisha wanapokuwa uwanjani wasifikirie matokeo yaliyopita bali kupambana kutafuta ushindi.

Chanzo: Mwanaspoti