Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting kujiuliza kwa Gwambina

83db4cc80436b38d2b684b9571d45808 Ruvu Shooting kujiuliza kwa Gwambina

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MICHEZO miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mzunguko wa 20, inatarajiwa kuendelea wakati Ruvu Shooting watakuwa na mtihani mgumu wa kusaka pointi tatu dhidi ya Gwambina mchezo utakaochezwa Uwanja wa Gwambina Complex leo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kwakuwa timu hizo michezo yao iliyopita zilifanya vibaya, Ruvu Shooting walipoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Namungo FC na Ihefu FC.

Gwambina wenyewe katika mchezo ulioita walitoka sare dhidi ya Kagera Sugar na kupoteza dhidi ya Biashara United, hivyo wanataka kurejesha imani kwa mashabiki wao.

Pia ushindani wa mchezo huo unatokana na utofauti wa nafasi wanazoshika kwenye msimamo, ambapo Ruvu Shooting wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 28 wakati wambina ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo wanakalia nafasi ya 15 wakiwa na pointi 20.

Kuelekea kwenye mchezo huo kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa alitamba kuibuka na ushindi ili kufuta makosa yaliyowafanya kupoteza michezo miwili mfululizo na alifanya kikao na wachezaji wake wote juu ya umuhimu wa kupata ushindi kurudisha morali.

“Mzunguko wa pili ni mgumu na michezo iliyopita tulifanya makosa kadhaa yaliyo tugharimu nimeshayafanyia kazi kwenye mazoezi yetu ya kila siku naamini utakuwa mchezo mzuri na wa ushindani tukipambana kutafuta pointi tatu,” alisema Mkwasa.

Mchezo mwingine mkali na wenye ushindani KMC watawaalika Mwadui FC mchezo utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

KMC wanaoshika nafasi ya sita wakiwa na pointi 25 wanahitaji ushindi ili kuongeza kasi yao na kuwania nafasi za juu kwenye msimamo, huku wakikutana na vibonde wa ligi hiyo, Mwadui FC wenye pointi 15.

Chanzo: habarileo.co.tz