Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu Shooting hoi kwa Singida Big Stars

Singida Vs Ruvu Sh.jpeg Ruvu Shooting walikubali kichapo cha goli 1-0

Sun, 27 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao la Frank Zakaria dakika ya 78 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya ya Tanzania Bara mchezo uliopigwa jana jioni Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanazidi kuwapa vijana wa Charles Mkwasa wakati mgumu wakihitaji nguvu ya ziada kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu msimu ujao.

Kwa ushindi huo, Singda Big Stars inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 13 na kurejea nafasi ya nne, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 11 za mechi 14 katika nafasi ya 13.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live