Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu, Mtibwa vita ya pointi tatu leo

Da6e32412455aa90b3caad16038bd99b.jpeg Ruvu, Mtibwa vita ya pointi tatu leo

Fri, 8 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya Ruvu Shooting imejipanga kuwapa furaha mashabiki wake kwa kushinda mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani leo.

Ruvu Shooting wanashika nafasi ya nne kwenye msimamo wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 16, wanaingia katika mechi hiyo wakitafuta ushindi ili kumaliza vizuri mzunguko wa kwaza vizuri.

Wanakutana na Mtibwa Sugar wanaoshika nafasi ya 10 wakiwa na pointi 22 baada ya kucheza michezo 17 wanahitaji ushindi kusahihisha makosa yaliyowafanya kupoteza mechi iliyopita kwa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na vikosi vyote kufanya vizuri mechi zilizopita, kwani Ruvu Shooting walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex Dar es Salaam.

Rekodi zinaonesha walipokutana mchezo wa raundi ya kwanza, timu hizo zilitoka suluhu katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kuelekea kwenye mchezo huo Kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa alisema maandalizi waliyofanya ni kutafuta ushindi kuwafurahisha mashabiki kwa kuanza mwaka mpya vizuri.

“Mchezo utakuwa mgumu lakini siku zote unapocheza nyumbani unakuwa na faida, wachezaji wangu wameandaliwa kwa kutafuta ushindi kuwafurahisha mashabiki iwe zawadi ya kuanza mwaka mpya,”alisema Mkwasa

Alisema jambo linalompa faraja ni kuona mapungufu yaliyojitokeza mchezo uliopita ameshayafanyia kazi na kilichosalia ni wachezaji kuonesha kwa kusaka ushindi.

Mchezo mwingine mkali leo, Mbeya City watawakaribisha KMC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Chanzo: habarileo.co.tz