Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rungu la FA lamsubiri Roberto De Zerbi

Brighton Roberto De Zerbi Kocha Mkuu wa Brighton, Roberto De Zerbi

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Brighton, Roberto De Zerbi huenda akakabiliwa na adhabu ya Chama cha Soka England (FA) kufuatia malalamiko yake dhidi ya waamuzi.

Kocha huyo kutoka nchini Italia aliwapiga vijembe waamuzi, John Brook na Andy Madley baada ya kutoa kadi nyekundu moja kwa moja kwa mchezaji wake, Mahmoud Dahoudm wakati timu yake ikiambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Sheffield United kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

De Zerbi alisema: “Mimi napenda kuzungumza ukweli asilimia 80 siwapendi waamuzi wa England. Sina jambo jipya zaidi, siwapendi kutokana na tabia zao uwanjani.”

Hivi karibuni kocha huyo amekuwa na mzozo na maafisa wakuu tangu kuwasili kwake katika ardhi ya Uingereza na anatajwa kuwa kocha mgumu zaidi kukabiliana naye kwenye ligi.

Kutokana na De Zerbi kuwakosoa waamuzi huenda FA ikampa adhabu lakini kwanza hadi uchanguzi utakapokamilika kwa mujibu wa gazeti la The Sun.

Baadhi ya watu wa ndani wa bodi ya waamuzi PGMOL wanahisi De Zerbi amevuka mipaka zaidi kutokana na kauli yake, hivyo hatua dhidi yake inahitajika kama kupigwa faini au kufungiwa.

Pia imeelezwa De Zerbi anaweza kuzingatia mkataba na sheria mpya iliyoanzisha msimu huu hata kama atalimwa faini na FA.

Mkataba huo, ni sehemu ya kampeni ya ‘Love Football Linda Game’ ambao unasema makocha wote lazima kuheshimu na kuwajibika zaidi.

Tabia ya makocha wakubwa kuwalalamikia marefa imeongezeka maradufu na kuleta hofu hususan kutokana na sheria hiyo mpya.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta aliwashutumu marefa baada ya kushindwa kuchezesha mechi ya ligi baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Newcastle, ingawa alimsifu mwamuzi Michael Oliver licha ya mchezaji wake Fabio Vieira kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley.

Chanzo: Dar24