Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rulani Mokwena anavyotumia vyema Ramani iliyoachwa na Pitso Mosimane

Rhulani Mokwena.jpeg Rulani Mokwena anavyotumia vyema Ramani iliyoachwa na Pitso Mosimane

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni rahisi sana kumaliza sifa zote kwa Rulani Mokoena kwa mafanikio ambayo Sundowns imefikia,si Wengi watakumbuka kuwa haya ni matunda ya "BLUE PRINT" iliyochorwa na Pitso Mosimane.

Kabla ya mwaka 2012 ambao Pitso aliwasili rasmi kama Head Coach,Sundowns ilikuwa kwenye kipindi cha kujitafuta ambapo walipitia makocha 8 katika kipindi cha miaka 6 kwa wastani wa kocha mmoja kila mwaka.

Haya yote yalibadilishwa na Pitso ambaye aliifanya Sundowns kuwa serious na mashindano ya Afrika mpaka walipotwaa kombe la kwanza mwaka 2016 wakiwafunga Zamalek.

Kama taasisi Sundowns walifanya kitu cha tofauti sana kudumu na kocha mzawa kwa miaka 8 huku wakimuwezesha kwa hali na mali na hata Pitso alipoondoka haikuwa kazi ngumu kufanya SUCCESION FROM WITHIN yaani kupata mrithi toka ndani badala ya kuleta mtu mpya.

Mafanikio huandaliwa na kwa hiki tunachokiona leo kwa Sundowns tujiandae kukiona kwa muda mrefu zaidi,mchumia Juani Hulia Kivulini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live