Christian Eriksen mara ya mwisho kuonekan uwanjani ni kwenye mashindano ya Euro 2020 alipopata tatizo la moyo kusimama na kumuweka nje kwa muda mrefu.
Eriksen amevunja mkataba na klabu yake ya Inter Milan kutokana na sheria za nchini italia kutokuruhusu mchezaji aliyepandikizwa kifaa maalumu cha kuweza kumsaidia mapigo ya moyo.
Ingawa kwa sheria za nchini italia Christian Eriksen haruhusiwi kucheza lakini anaweza kuendelea kucheza sehemu nyingine barani ulaya kwani sheria zilizopo nchini Italia zinatofautiana kwenye nchi kama Uingereza, Uholanzi na Denmark.
Chama cha soka nchini Uingereza kimethibitisha kuwa idara yake ya “sports cardiologist” inamchukulia mchezaji ni kama mchezaji mwengine maamuzi ya kama ataendele kucheza au kustaafu hayo ni maamuzi binafsi, pia FA wamethibitisha kuwa wanasimamia wachezaji karibia 1500 kwa mwaka.
Kwa sasa Christian Eriksen yuko nchini kwao Denmark akiwa anafanya mazoezi na klabu yake ya zamani, kuendelea au kutoendelea kucheza soka sasa ni maamuzi yake binafsi.