Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rufaa ya Barcelona kwa Lewandowski yagonga mwamba

Barca Lewandowski Appeal.png Rufaa ya Barcelona kwa Lewandowski yagonga mwamba

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Nchini Uhispania RFEF limetupilia mbali rufaa ya klabu ya Barcelona ya kupinga adhabu ya mshambuliaji Robert Lewandowski ya mechi tatu ambaye alioneshwa kadi nyekundu katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Osasuna.

Awali Lewandowski alioneshwa kadi ya pili ya njano ambayo alipaswa kukosa mechi moja lakini RFEF imemuongezea adhabu ya mechi mbili zaidi kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu kwa refa baada ya kumwonesha ishara ya dole puani wakati anatolewa kwa kadi nyekundu jambo ambalo limetafsiriwa vibaya na RFEF.

Lewandowski ambaye ni kinara wa magoli Ligi kuu Uhispania akiwa na magoli 13 atakuwa nje katika mechi ya derby dhidi ya Espanyol, sambamba na mechi dhidi ya Atletico Madrid na Getafe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live