Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rudiger: Siogopi Fainali UEFA, namuogopa Mungu

Rudiger Amuogopa Mungu Beki wa Real Madrid, Anton Rudiger

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Real Madrid wakijiandaa kuwavaa Borussia Dortmund Juni 1 katika mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Mlinzi wa Real Madrid amesema kuwa Dortmund sio kitu anachokiogopa kabisa katika mipango yake.

Akizungumza Ridiger anasema;

"Unadhani ninahofu kuhusu final ya UEFA champions league dhidi ya Borusia Dortmund ? Hapana nadhani katika maisha yangu nina muhofia Mwenyezi Mungu pekee mana mwisho wa siku sisi sote ni binadamu na hakuna sababu yoyote ya msingi ya kunifanya nimuogope binadamu kama mimi"

"Mimi ni Muislamu na nina imani kubwa ndani ya dini yangu na hii ni sababu tosha kwamba napaswa kumuogopa mwenyezi Mungu pekee sababu ndio muumba wa kila kitu Kwahio hatupaswi kuwa na sababu ya kumuogopa binadamu mwenzio".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live