Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruben Neves ampagawisha Thomas Tuchel

Ruben Neves Ruben Neves

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Mabingwa wa Soka Barani Ulaya Chelsea FC, Thomas Tuchel ameripotiwa kumuwania kiungo wa Wolves, Ruben Neves wakati wa Dirisha Dogo (Januari 2022).

Tuchel anataka kuboresha safu yake ya kiungo baada ya N’Golo Kante na Mateo Kovacic kukosa sehemu kubwa za michezo ya Ligi Kuu msimu huu, huku Saul Niguez akiwa bado hajaanza kuonyesha makali yake.

Taarifa zinaeleza kuwa Neves, ameweka kwenye orodha ya wachezaji ambao wanapigiwa chepuo na meneja huyo kutoka nchini Ujerumani, ili asajiliwe huko Stamford Bridge.

Kutokana na hilo, Todofichajes linaripoti kwamba Tuchel anamwona Neves ni mtu sahihi wa kunaswa kwenye kikosi chake.

Hata hivyo, Wolves hawapo tayari kumwaachia staa wao huyo katikati ya msimu na wanaweza kukaa mezani kujadili hilo kama itawekwa mezani ofa inayofikia Pauni Milioni 40.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live