Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roy Keane atupa kijembe kwa Man United, awapongeza Chelsea

D5EB9053 CCAA 4288 833F E07D5BA4B3F3.jpeg Roy Keane anapendezwa zaidi na mbinu za Potter kuliko Ten Haag

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Roy Keane amedai kwa sasa kocha mpya wa klabu ya Chelsea Graham Potter kuliko yule wa timu yake ya Manchester United Eric Ten Haag.

Gwiji huyo aliehudhuria katika kipindi cha Monday Night Football alionesha kuvutiwa na kocha wa klabu ya Chelsea Graham Potter kwa namna anavyofundisha na aina yake ya mchezo ndio kitu kinachomvutia Roy Keane.

Wakati gwiji huyo akiwa kwenye kipindi hicho na kuulizwa makocha bora katika ligi kuu ya Uingereza na gwiji huyo aliwataja Pep Guardiola wa Man City, Thomas Frank anayefundisha Brentford pamoja na Graham Potter wa Chelsea na kutomtaja kocha wa United kitu kilichowashangaza watu wengi.

Roy Keane amekua akisifika mara nyingi kwa kusema ukweli na kua na msimamo wa kile anachokiamini na kauli yake imeweza kuchukua nafasi kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki wa klabu ya Man United wakionesha kuchukizwa na kauli ya gwiji huyo.

Pia gwiji huyo aliweza kutaja wachezaji wake watatu bora wa muda wote akiwataja Cristiano Ronaldo,Diego Maradonna, pamoja na Zinedine Zidane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live