Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roy Keane amuwashia moto Ten Hag

TEN HAG KEANE.png Roy Keane amuwashia moto Ten Hag

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Manchester United, Roy Keane alimwambia Erik ten Hag ajiuzuu baada ya kucheza hadharani ndani ya uwanja wa Wembley wikiendi iliyopita.

Ten Hag alikuwa akicheza sambamba na wachezaji wake Antony na Lisandro Martinez baada ya kuvunja ukame makombe kwa mara ya kwanza baada ya miaka sita.

Aidha kwa mujibu wa Keane alizungumza hivyo kama utani tu huku akimsifia Ten Hag kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo kwa muda mfupi.

Ten Hag alikiongoza kikosi chake katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle uliyochezwa uwanja wa Wembeley wikiendi iliyopita.

Aidha Mkongwe huyo alimwambia maneno hayo mbele ya wachambuzi wa soka wa kituo cha televisheni cha Sky Sports akiwemo Gary Neville.

Inafahamika Keane hapendi masihara kwenye soka kama kucheza muziki uwanjani, aliwahi kuwaponda wachezaji wa Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia Qatar.

Baada ya Ten Hag kuuangana nao katika mahojiano na Sky Sports Keane akazungumza wazi kabisa akimtaka kocha huyo aachie ngazi kufuatia kitendo hicho.

"Ten Hag unatakiwa kujiuzulu usiku huu," naye Ten Hag akamjibu " Niliwahi kufanya hivyo nilipokuwa Ajax baada ya kubeba ubingwa wa ligi, matumaini nitaendelea utamaduni huu pamoja na wachezaji wangu Martinez na Antony,"

Ten Hag aliwahi kucheza muziki uwanjani kwenye mechi yake ya mwisho ya ligi Ajax ikibeba ubingwa, Mholanzi huyo alicheza pamoja na wachezaji wake hao wa zamani wa Ajax. Kitendo hicho ni kama kukumbushia mafanikio yao waliyowahi kupata wakati walipokuwa Ajax.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live