Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roy Keane amkosoa Carrick , Kisa sare na Chelsea

Roy Keane.png Kiungo wa zamani wa Man United, Roy Keane

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Roy Keane, amesema Manchester United jana haikucheza vizuri kama alivyosema msimamizi wa Manchester United kwa sasa Michael Carrick.

Akizungumza katika kipindi cha michezo cha Sky Sport, Roy Keane alisema hakuna plan yoyote kwa United wala mabadiliko kama alivyosema Carrick, huku akimshauri kocha ajae wa Manchester United Ralph Rangnick kutimua benchi la ufundi la sasa.

“Unaposema una plan, unaposema unajivunia timu ilivyocheza leo sio kweli, Carrick alikua pamoja na Solskjaer, timu imekua mbovu kwa muda wote hizo plan kazipata baada ya Ole kuondoka? lakini uzuri ambao anasema timu ilikua nao leo ni upi ?alisema Roy Keane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live