Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Rotation' ya mwisho ya Gamondi ni Ihefu

Faridi Muda 'Rotation' ya mwisho ya Gamondi ni Ihefu

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Nassredine Nabi ambaye kwa sasa yupo nchi Morroco akiinoa FAR Rabat aliweza kuifanya Yanga SC kuwa na Kikosi kipana, kila mchezaji alipata game time.

Gamondi anauwa vipaji vya wachezaji wengi, yeye anawachezaji wako special, mchezaji kama Mudathir Yahya, Faridi Mussa, Sure Boy sio wakupigwa benchi kila mechi.

Gamondi anamengi ya kujitafakari juu ya kukuza vipaji na kuwapa game time baadhi ya wachezaji.

Baadhi mashabiki wa yanga ambao hawajui au mapenzii na timu yao wataanza kupinga na siku wachezaji muhimu wakipata majeraha ndipo ataona shughuli yake itakavyokua.

Nabi hata akipata majeruhi watatu alikuwa hapati presha sana kwa sababu kikosi chake kilikuwa hakizidiani sana game fitness sababu kila mchezaji alikuwa akipata nafasi angalau kila baada ya michezo miwili.

Rotation ya mwisho ya Gamondi ilikuwa ni ile ya wachezaji saba kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ihefu ambapo alipoteza kwa bao 2-1, baada ya hapo Gamondia akaona isiwe tabu, nitacheza na cream players tu, wengine sugueni benchi.

Madhara yake ni kwamba, hata hawa wanaocheza kila mechi itafika wakati watachoka, watashindwa kumpa matokeo chanya wakati huo wale aliowaacha benchi tayari viwango viyakuwa vimeshuka na hawatakuwa na msaada tena kwenye kikosi, Gamondi achague yeye kufurahi sasa na kulia baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: