Kocha wa Klabu ya Simba, Robertinho amesema kuwa mchezo wa kesho dhidi ya Vipers FC ni muhimu mno sio tu kwa timu bali pia kwa mashabiki na taifa.
Mbrazil huyo ameongeza kwa kusema watawashangaza kwenye mechi hiyo ya kesho Februari 25, ambayo Mnyama yupo ugenini nchini Uganda kuwavaa Vipers FC Ligi ya Mabingwa Afrika
"Ni mchezo muhimu kwa Klabu, mashabiki popote walipo na Taifa, ninakiamini kikosi changu, ndiyo tuna siri pengine kesho tutawashangaza kwa kuanzia."
"Lakini narudia tena kusema kwenye Champions League hakuna mchezo rahisi, kinachotakiwa ni alama tatu, tunahitaji point tatu, tunahitaji ushindi na hilo ndiyo lengo letu."
"Nina waheshimu sana Vipers lakini Simba inakuja kwa kuwaheshimu wapinzani na kushinda kuvuna alama tatu."
Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameyasema hayo leo kwenye mkutano wake na wanahabari nchini Uganda kabla ya kutupa karata yake muhimu mbele ya Vipers FC ili kufufua matumaini ya kusonga mbele baada ya kuburuza mkia kwenye kundi C ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.