Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rooney autaka Ukocha Man United

Wayne Rooney.jpeg Wayne Rooney

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza Wyne Rooney kwenye mahojiano maalum na shirika la utangazaji la Uingereza BBC amesema moja kati ya ndoto zake ni kufundisha klabu yake hiyo ya zamani pamoja na Everton.

“Bila shaka hilo ndilo lengo langu, Manchester United na Everton ni zote hizi ni kazi ninazojaribu kufika kuzifanya” alisema Rooney alipoulizwa kuhusu lengo la kuifundisha United.

Rooney tangu kustaafu kwake mwaka 2021 alianza kujikita kwenye ukocha na hadi sasa amefundisha timu za Deby County, DC United na Birmingham City ambapo kote alikuwa akitimuliwa kwa kupata matokeo mabaya huku akiwa na takwimu hizi, michezo 152, kushinda 41, kupoteza 73 na sare 38.

Je kwa uzoefu na takwimu hizo anafaa kufundisha United? weka maoni yako hapo chini

Chanzo: www.tanzaniaweb.live