Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rooney atupiwa virago DC United

Rooney DC United Wayne Rooney

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya DC United inayoshiriki Ligi Kuu ya MLS ya Marekani imethibitisha kuachana na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney kama kocha mkuu klabuni hapo kwa makubaliano ya pande zote.

Rooney aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu klabuni hapo mnamo Julai 12, 2022, alipojiunga na klabu hiyo baada ya kuinoa klabu Derby County ya England kwa miaka miwili.

Rooney pia amewahi kuichezea DC United alipojiunga nayo mnamo Juni 2018 akiichezea mechi 48 na kufunga mabao 23 na kusaidia (assist) mengine 15

Chanzo: www.tanzaniaweb.live