Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rooney aiweka Birmingham anga za Man City

Skysports Wayne Rooney Birmingham 6317763.png Rooney aiweka Birmingham anga za Man City

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mpya wa Birmingham City, Wayne Rooney anaamini timu yake inaweza kuiga mabadiliko ya maendeleo ya soka la Manchester City na Newcastle United.

Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United na England amerejea katika soka la England baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Mmiliki wa Birmingham ambaye ni raia wa Marekani pamoja na mtendaji mkuu, Garry Cook walikuwa mstari wa mbele kumchagua Rooney katika kinyanganyiro cha ukocha.

Rooney alijiamini atapata kazi ya ukocha Birmingham akachukue nafasi ya John Eustace ambaye kibarua chake kilikuwa hatarini.

“Katika Ligi Kuu England tumeona Manchester City na Newcastle jinsi wanavyoendeleza soka. Klabu hizi zilimilikiwa na wawekezaji tofauti, kwa sasa wamepata wawekezaji sahihi ndio wamepata mafanikio makubwa. Naamini soka la klabu yetu litabadilika. Naamini tutapanda daraja kutoka Championship. Halafu tutakaa chini na kutengeneza timu. Kama shabiki wa soka najua kitu kinachofuata.”

Pia Rooney alitoboa siri kuwa alipokea ofa zilizotumwa na klabu sita za England baada ya kuondoka DC United, lakini akaamua kuichagua Birmingham.

Wakati huohuo rais na mtendaji mkuu wa Ligi ya Kuu Saudi Arabia, ambaye pia ni mtendaji mkuu wa Birmingham, Cook alitoboa siri kuwa Rooney alipiga chini ofa kutoka Saudia.

Wiki iliyopita Rooney alikuwa na mazungumzo na mabosi wa Birmingham City kwani alijitokeza hadharani baada ya jina lake kupendekezwa.

Chanzo: Mwanaspoti