Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rooney Aliwakataa Everton

Rooney Wayne.jpeg Kocha wa Derby County, Wayne Rooney

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Everton wakiendelea kuhaha kutafuta kocha wa muda mrefu, Wayne Rooney amethibitisha kuikataa nafasi ya kwenda Goodison Park.

Everton wameachana na Rafa Benitez na sasa, timu ipo chini ya Duncan Ferguson kama muangalizi wa muda. Wakati huu huu, uongozi wa klabu hiyo unaendelea kumtafuta kocha wa muda mrefu atakayeiongoza timu hiyo.

Wakati mchakato ukiwa unaendelea, Wayne Rooney amethibitisha kupokea taarifa ya Everton kutaka kuzungumza nae kuhusu nafasi ya ukocha kwenye klabu hiyo. Wayne anasema alipata taarifa hizo kupitia kwa wakala wake.

Hata hivyo, Wazza alikataa nafasi hiyo ya kuzungumza na Everton akiamini kuwa, bado ana kazi kubwa ya kufanya na waajiri wake wa sasa, Derby County na hivyo, haoni kama ni muda sasa kwake kuondoka klabuni hapo.

Anajiamini kuwa ana uwezo wa kufundisha timu za EPL na endapo Everton au timu yeyote itamuhitaji kwa hapo baadae, hatosita kukaa nao mezani na kuzungumza lakini, huu sio wakati sahihi kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live