Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronwen Williams asaini mkataba mpya Mamelodi

IMG 6868.jpeg Ronwen Williams asaini mkataba mpya Mamelodi

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mamelodi Sundowns imetangaza kumuongeza mkataba wa miaka minne kipa wake mzawa, Ronwen Williams ambao utamfanya adumu Chloorkop angalau mwaka 2028.

Mkataba huo unatoa fursa kwa Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ aliyejiunga na Mamelodi Sundowns mwaka 2022 kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Ronwen Williams amekuwa na msimu mzuri akiiwezesha Mamelodi kutwaa mataji ya Ligi Kuu ya DStv, African Football League (AFL) na kufuzu kwenye michuano ijayo ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.

Alifanya vizuri pia kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) akishinda Tuzo ya Kipa Bora wa michuano hiyo baada ya kuiwezesha Bafana Bafana kumaliza nafasi ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live