Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo tatizo United

Ronlado Problem Wachezaji United wakerwa na Ronaldo

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Mkuu wa Soka wa Bild Christian Falk, anadai baadhi ya wachezaji wanadaiwa kutofurahishwa na tabia ya Ronaldo kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Kufuatia ripoti mbalimbali kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mpasuko kati ya wachezaji wa Manchester United, Marcus Rashford hakusita kutupilia mbali uvumi kwenye Twitter kuhusu baadhi ya wachezaji kutoridhika na tabia ya Cristiano Ronaldo.

Licha ya kuwasili kwa nyota huyo wa Ureno, Mashetani Wekundu wameshindwa kufanya vizuri chini ya Ole Gunnar Solskjaer na kocha wa muda Ralf Rangnick, ambaye alichukua nafasi baada ya kutimuliwa kwa Ole.

“Wachezaji wa Kiingereza kama Harry Maguire, Marcus Rushford na wenzao wamekasirishwa kwamba Ronaldo anataka kuongoza chumba cha kubadilishia nguo na kundi lake,” Falk alichapisha kwenye Twitter.

“Kuna hatari ya mgawanyiko katika timu.”

Kufuatia taarifa hiyo Rashford hajataka kugombanishwa na CR7 ameamua kupangua madai hayo na kusisitiza kuacha kuleta magawanyo ndani ya timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live