Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo na safari ya matumaini leo

Ron Cristiano Ronaldo

Thu, 24 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo leo atakua dimbani kuiwakilisha timu yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Ghana katika mchrzo wa kwanza wa kundi H.

Nyota huyo ambaye anakwenda kushiriki michuano hiyo kwa mara tano sasa huku ikiwa ni wazi haya yatakua mashindano yake ya mwisho kwenye ngazi ya timu ya taifa, anahitaji kupambana ili kuweza kutimiza ndoto yake ya kubeba taji la kombe la dunia.

Ronaldo ambaye tayari ameshatwaa mataji mawili na timu ya taifa ya Ureno ikiwemo lile la Euro 2016 huku deni kubwa ni kombe la dunia ambalo ndio safari ya matumaini inaanza leo dhidi ya Ghana ili kuangalia kama ataweza kutimiza ndoto zake.

Timu ya taifa ya Ureno ni miongoni mwa timu iliyobarikiwa kua na vipaji vya hali ya juu kwenye kikosi chake japokua haizungumzwi sana, Lakini ni timu ambayo imejumuisha wachezaji bora na nguli ambao wanakipiga katika timu tofauti tifauti barani ulaya tena kwa ubora mkubwa.

Huku Ronaldo na vijana wake wakiwa wanatazamia kuanza safari yao ya matumaini ili kubeba taji la dunia timu ya taifa ya Ghana ni miongoni mwa timu kutoka Afrika ambayo mara nyingi hua inajitahidi kufanya vizuri kwenye kombe la dunia. Hivo mchezo huo unatarajiwa kua wenye ushindani na ubora mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live