Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo kwenye tizi zito Saudi Arabia

Ronaldo Tizi Nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mwenye njaa katika mazoezi huku mchezaji mwenzake wa Al-Nassr, Abdulrahman Ghareeb akifunguka kuhusu maisha “siriazi” ya fowadi huyo.

Akizungumza na mtayarishaji wa maudhui, Abu Mashael, Ghareeb alisema:

“Maisha ya Ronaldo ni mazito sana. Hukasirika ikiwa atashindwa katika mazoezi licha ya kushinda mataji mengi ya Ulaya na tuzo binafsi. Hii ni pamoja na kuhudhuria mazoezi mapema kabla ya wengine wengi, napokea sapoti kubwa kutoka kwa Ronaldo. Anasimama nami sana na ndiye sababu ya mimi kuhudhuria mazoezi kwa shauku kubwa.”

Ronaldo hatakuwa peke yake mwenye uzoefu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika Ligi ya Saudi Pro msimu ujao, huku nchi hiyo ikijitahidi kujenga ligi ya magwiji wa dunia kabla ya msimu wa 2023-24. Anayeshikilia tuzo ya Ballon d’Or 2022, Karim Benzema amekamilisha uhamisho kwenda Al-Ittihad..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live