Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo kuwakosa West Ham

Cr Ronaldo Cristiano Ronaldo

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Cristiano Ronaldo ana wasiwasi wa kuukosa mchezo dhidi ya West Ham kutokana na matatizo ya shingo.

Ronaldo alikosa michezo miwili kwa tatizo la misuli na alirejea kwenye mchezo wa siku ya jumatano dhidi ya Brentford na Man Utd kushinda kwa 3-1, kulitokea sintofahamu baada ya kutolewa nje huku mreno huyo akionekana kutoridhika.

Kocha wa United Ralf Rangnick alielezea hilo kwenye kituo cha klabu hiyo MUTV,

“Cristiano ni swali ambalo bado tunajiuliza kwa sababu ana matatizo ya shingo, alianza matibabu jana kwa masaa mawili au matatu, kwa hiyo tutaangalia hali yake kwa siku ya leo.

“Edinson Cavani bado hajaanza mazoezi na timu na tunatarajia kusimamisha mazoezi leo na tutaangalia jinsi ya kufanya maamuzi ya mwisho baada ya kumaliza mazoezi leo, kama atakuwepo kwenye mchezo wakesho.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live