Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo kutambulishwa rasmi kwa Mashabiki wa Al Nassr

Ronaldo Al Nassir Leo Cristiano Ronaldo

Tue, 3 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cristiano Ronaldo atatambulishwa rasmi na klabu ya Al-Nassr mbele ya umati wa mashabiki katika uwanja wa Mrsool Park, unaomilikiwa na klabu hiyo uliyopo ndani ya jiji la Riyadh, Saudi Arabia ambao unaingiza mashabiki 25,000.

Ronaldo aliwasili jana Saudi Arabia pamoja na familia yake akiambatana na watu wa mambo ya kiufundi na waandishi wa habari.

Ronaldo atakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa duniani kukipiga katika klabu hiyo kwenye historia ya maisha yake ya soka. Vile vile waziri wa michezo wa Saudi Arabia Abdulaziz bin Turki Al-Feisal ameahidi atazisapoti klabu zote nchini humo endapo madili makubwa yatatokea.

Klabu ya Al-Nassr mabigwa mara tisa wa Ligi Kuu Saudi Arabia baada ya utambulisho wa Ronaldo, walisema wametengeneza historia kubwa baada ya kukamilisha uhamisho wa staa huyo aliyeondoka Manchester United, baada ya mkataba wake kuvunjwa siku chache tu baada ya mahojiano na Morgan Piers kupitia kituo cha televisheni akiiponda klabu yake.

Kabla ya kurejea Man United akitokea Juventus, Ronaldo aliichezea Madrid kuanzia msimu wa 2009-2018 na kufunga mabao 450 katika mechi 438 alizocheza.

Mreno huyo aliondoka Man United na kujiunga na Al Nassr kwa mkataba wa miaka miwili na nusu, baada ya kuwaponda wamiliki wa klabu familia ya Glazer kupitia mahojiano na mtangazaji maarufu Piers Morgan.

Ronaldo, 37, amekubali mkataba wa miaka miwili na nusu kwenye klabu hiyo ya Saudi Arabia, ambapo kwa mwaka atakuwa akiweka kibindoni Pauni 173 milioni sawa na Shilingi ya Kitanzania 484,958,790,000 (Sh485 Bilioni).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live