Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo aweka rekodi, Man U ikishinda kibabe

Ronald Scores Mshambuliaji wa United,Cristiano Ronaldo akishangilia Goli dhidi ya Villareal

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Goli la dakika za lala salama lililofungwa na Mshambuliaji Cristiano Ronaldo, limeiwezesha Manchester United kuondoka na pointi tatu katika uwanja wa Old Trafford dhidi ya Mabingwa wa Uropa msimu uliopita Villareal.

Goli hilo lililofungwa dakika ya 90+5, lilitosha kuihakikishia ushindi United baada ya kuonekana kama mechi hiyo inakwenda kumalizika kwa sare.

Katika mchezo huo wageni ndio waliotangulia kupata goli dakika ya 53 kupitia kwa mshambuliaji P. Alcacer, kabla ya beki wa kushoto wa Man United , A. Telles kuisawazishia United dakika ya 60 kwa shuti kali la mguu wa kushoto.

Mchezo ulibaki hivyo mpaka dakika za 90+5 ambapo Cristiano Ronaldo alifunga bao la ushindi akimaliza pasi safi ya Jesse Lingard, na kufanya mchezo huo kuisha kwa united kushinda 2-1.

Katika mechi hiyo ilimshuhudia nyota kutoka Ureno, Cristiano Ronaldo akicheza mechi yake ya 178, na kumfanya kuwa mchezaji aliecheza mechi nyingi zaidi katika historia ya mashindanoo ya Ligi ya Mabingwa akifuatiwa na Mkongwe kutoka Hispania, golikipa Iker Casillas aliecheza mechi 177.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo F, Atalanta wameshinda goli 1-0 dhidi ya Young Boys.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live