Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo atoka kapa Saudia, aangua kilio hadharani

Ronaldo Kilio Ronaldo aangusha kilio baada ya kukosa Ubingwa

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al Hilal kutoka Saudi Arabia imefanikiwa kutwaa Kombe la Mfalme la Mabingwa kwa Msimu wa 2023/24 baada ya kuichapa Al Nassr kwa mikwaju ya Penati 5-4.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 120 za kawaida na kulazimika kwenda hatua ya matuta.

Ubingwa huo unakamilisha jumla ya makombe 11 kwa Al Hilal tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1957 huku Al Ahli akiwa anaongoza mbio za kutwaa kombe hilo ambalo amelitwaa mara 13.

Staa Cristiano Ronaldo alijikuta akiangua kilio mara baada ya mchezo ikiwa amemaliza msimu huu pasipo kubeba taji lolote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live