Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo atoa tamko baada ya kusimamishwa Manchester United

Ronaldo Hj Cristiano Ronaldo

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa Cristiano Ronaldo kupitia ukurasa wake Instagram baada ya Manchester United kumuondoa kama sehemu ya kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Chelsea.

“Kama nilivyofanya siku zote katika taaluma yangu, najaribu kuishi na kucheza kwa heshima kwa wenzangu, wapinzani wangu na makocha wangu. Hilo halijabadilika, sijabadilika.

"Mimi ni mtu yule yule na mchezaji yuleyule ambaye nimekuwa kwa miaka 20 iliyopita nikicheza soka la kulipwa na heshima imekuwa jukumu muhimu sana katika mchakato wangu wa kufanya maamuzi.”

“Nilianza mdogo sana, mifano ya wachezaji wakubwa na wazoefu ilikuwa muhimu sana kwangu wakati wote. Hivyo siku zote nimejaribu kujiweka kama mfano kwa vijana waliokua katika timu zote ambazo nimewakilisha.

"Kwa bahati mbaya hilo haliwezekani wakati wote na wakati mwingine hasira za muda hutulemea. Hivi sasa, ninahisi tu kwamba ni lazima niendelee kufanya kazi kwa bidii Carrington, kusaidia wachezaji wenzangu na kuwa tayari kwa kila kitu katika mchezo wowote.

"Kukata tamaa kutokana na shinikizo sio chaguo. Haijawahi kuwa chaguo. Hii ni Manchester United, na kwa umoja lazima tusimame. Hivi karibuni tutakuwa pamoja tena.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live