Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo atishia kuondoka Man United

Ronaldo Kesi Ronaldo

Fri, 24 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United na Timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amesema anaangalia mwenendo wa klabu yake katika dirisha la usajili ili kutathmini kama anaweza kuendelea kubaki klabuni hapo au kutimka.

Kwa mujibu wa jarida la Record_Portugal mchezaji huyo ambaye ndiye kinara wa ufungaji bora wa mabao katika historia ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya pamoja na mfungaji bora wa muda wote wa Timu ya Taifa ya Ureno anatarajia kuwa Manchester United itasajili wachezaji wenye kiwango cha juu kwa ajili ya kuongeza nguvu na kuipa timu hiyo nafasi ya kurejea katika mashindano ya klabu bingwa barani humo.

Tayari kumekuwa na baadhi ya taarifa zikimhusisha nyota huyo kupewa kitambaa cha unahodha wa klabu hiyo katika utawala mpya wa kocha raia wa Uholanzi Eric Ten Hag ambaye anatazamiwa kufanya mabadiliko makubewa ndani ya kikosi hicho kilichoshindwa kukata tiketi ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live