Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo atabaki Man United Msimu Ujao?

RONALDO 7777 Ronaldo ameonesha nia ya kuondoka kusaka timu atakayopata nafasi ya kucheza UEFA

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo jana alijumuishwa kwenye kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu kutoka nchini Hispania Rayo Vallecano kwenye dimba la Old Trafford.

Baada ya sintofahamu kuhusu hatma ya mchezji huyo wa kimataifa kutoka nchini Ureno kwenye viunga vya Old Traford hatimaye jana kavaa jersey na kufanikiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kutoka na nafasi kuchukuliwa na Amad Diallo.

Ronaldo hakusafiri na timu kwa ajili ya michezo ya kujianda na msimu huu kutokana na sababu za kifamilia ambazo klabu ilitoa taarifa na na kupelekea kukosa mchezo didi ya Liverpool nchini Thailand na ule wa atlatico madrid jijini Oslo.

“Ronaldo atakuwepo kwenye kikosi. Na tutaangalia ni muda gani anaweza kucheza,” Kabla ya mechi Ten Hag aliuwambia mtandao wa klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amebakisha mwaka mmoja kwenye kandarasi yake, na yuko tayari kusamee kitika cha mshahara wake ili aweze kuhama klabu hiyo.

Man Utd msimu uliyoisha ilifanikiwa kumaliza nafasi ya sita kwenye ligi kuu nchini Uingereza, na kupelekea kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani, sasa wanatarajia kwenda Kushiriki michuani ya Europa League msimu huu na wataanzia mzunguko wa pili.

Ronaldo tayari amekwishaonesha nia ya kusaka timu nyingine itakayomfanya akashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, lakini kubwa ni tabia aliyoionesha kwenye mchezo wa jana alipotolewa na kuondoka moja kwa moja uwanjani.

Je Ten Hag atafanikiwa kumshawishi Ronaldo aendelee kubaki kwa msimu mmoja zaidi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live