Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo apigwa faini Uingereza

Ronaldo Cmu.jpeg Ronaldo apigwa faini Uingereza

Thu, 24 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Soka nchini Uingereza (FA) imemfungia Cristiano Ronaldo kucheza mechi mbili na kulipa faini ya pauni 50,000 (sawa na Tsh milioni 141) kwa kuvuta simu kutoka mikononi mwa shabiki mwenye usonji na kuitupa chini.

Ronaldo (37) ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Manchester United kuvunjwa amehukumiwa kwa; “Kufanya kitendo kisichofaa ama ujeuri...” kufuatia tukio lililotokea mwezi Aprili mwaka huu.

FA inatarajia kutangaza rasmi hukumu hiyo jioni ya leo, pia watatoa maelezo kamili ya sababu zilizowapelekea kufikia uamuzi huo.

Hii ina maana kuwa Ronaldo atafungiwa mechi mbili ikiwa atajiunga na klabu nyingine ndani ya Ligi ya England.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live