Cristiano Ronaldo anasema kitendo alichofanya cha kuondoka Old Trafford kabla ya kumalizika kwa mechi dhidi ya Tottenham siku ya Jumatano ni 'kubebwa na hisia' tu na kuwa siku zote anajaribu kuwa mfano bora.
"Siku zote nimejaribu kujionyesha mfano kwa vijana ambao walikua katika timu zote ambazo nimewakilisha," aliandika kwenye Instagram mnamo Alhamisi. "Hiyo haiwezekani kila wakati."
Aliongeza kuwa "Wakati mwingine hisia za wakati kutupata mahali ambapo hukutarajia.''
"Ninahisi tu kwamba lazima niendelee kufanya kazi kwa bidii Carrington, kuwaunga mkono wenzangu na kuwa tayari kila kitu katika mchezo wowote. "Kukubali shinikizo sio chaguo. Haijawahi kuwa hivyo. Hii ni Manchester United, na kwa umoja lazima tusimame. aliongeza Ronadlo.
United imesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 anasalia kuwa sehemu muhimu ya kikosi lakini wanachukulia hili kama suala la kinidhamu na hivyo hatoshiriki mechi ijayo dhidi ya Chelsea huko Stamford Bridge.
Vyombo vingi vya habari vinaripoti kuwa alikataa kucheza kama mchezaji wa ziada dakika za mwishonni dhidi ya Spurs.
Ronaldo alitoka kwenye benchi na kuteremka kwenye handaki katika dakika ya 89, ingawa United walikuwa wamefanya mabadiliko matatu pekee kati ya matano yaliyoruhusiwa.
Kwa muda mfupi aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kuondoka uwanjani.
Meneja Erik ten Hag alisema baadaye kwamba "atashughulikia" suala hilo siku ya Alhamisi.
Ronaldo pia alionyesha kutofurahishwa na kubadilishwa wakati wa sare ya 0-0 Jumapili nyumbani na Newcastle.
Mshambulizi wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Gary Lineker alisema tabia ya Ronaldo iliondoa juu ya kiwango cha kuvutia cha United dhidi ya Spurs. "Hilo halikubaliki - ni mbaya sana," Lineker alisema kwenye BBC.
Mlinzi wa zamani wa England, Micah Richards alisema: "Kwa mmoja wa magwiji wa mchezo kufanya hivyo wakati timu yako inaposhinda, kufanya hivyo kuhusu yeye, inakatisha tamaa."
Richards alisema tabia ya Ronaldo ni "haikubaliki" na anapaswa kuruhusiwa kuondoka katika dirisha la usajili la Januari.
"Meneja wake alikuwa na matatizo naye mwanzoni mwa msimu, wakati maandalizi, na kuendelea na hili... Nafikiri kuna njia moja tu hii inahitaji kufanywa sasa," Richards aliiambia BBC Radio 4. "Wanahitaji kufikia makubaliano Januari na wanahitaji kumwachia.