Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo aondoka Old Trafford baada ya kufanyiwa sub

Ronaldo Sepa Ot.jpeg Ronaldo akiondoka

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Cristiano Ronaldo ameichezea Manchester United mechi ya kwanza baada ya kukosekana kwa zaidi ya mwezi mmoja, pamoja na hivyo alicheza kwa dakika 45 dhidi ya Rayo Vallecano kisha akaondoka uwanjani wakati kipindi cha pili kikiendelea na kwenda kupanda gari lake kisha kuondoka kabisa uwanjani hapo.

Mashabiki walimpiga picha akitoka Uwanja wa Old Trafford, wapo walioamini alicheza mechi hiyo ili kujiweka fiti kwa kuwa anaondoka, wengine wakatafsiri ni utovu wa nidhamu kwa klabu na wachezaji wenzake.

Katika mchezo huo wa kirafiki ni #Ronaldo pekee ndie aliyefanyiwa mabadiliko wakati wa mapumziko, huku mchezo ukimalizika kwa matokeo 1-1.

Ronaldo amekuwa akihusishwa kuondoka Man United kwa sababu haijafuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA Champions League) msimu huu hivyo anasaka timu ambayo ataweza kushiriki michuano hiyo huku ikidaiwa kuwa Michuano ya Europa ambayo Man United atashiriki, sio hadhi ya Ronaldo.

Kocha wa #ManUnited, Erik ten Hag hakuzungumzia suala hilo la Ronaldo kuondokauwanjani wakati mechi ikiendelea. Si hivyo tu, haijaelezwa pia iwapo alikuwa na ruhusa ya kuondokauwanjanihapo.

Ikumbukwe kuwa, katika maandalizi ya msimu mpya, Ronaldo aliondoka kikosini na hakuwa na kikosi chake huku ikidaiwa kuwa alikuwa akisaka timu mbadala atakayoitumikia msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live