Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ronaldo anataka mabao 1,000

Cristiano Ronaldo 1000.jpeg Ronaldo anataka mabao 1,000

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amesema anataka kufikisha mabao 1,000 kabla ya kustaafu soka.

hiyo ilikuja baada ya staa huyo wa Al-Nassr kuendeleza rekodi yake baada ya kufunga mabao 125 kimataifa Ijumaa usiku.

Mreno huyo alifunga mabao mawili na kuisaidia Ureno kuibuka na ushindi wa 3-2 katika mechi yao ya kufuzu Euro 2024 dhidi ya Slovakia, ikiwa pia ni mechi yake ya 200 kwa timu ya taifa.

Mchezaji huyo (38) alivunja rekodi ya mkongwe Ali Daei mwaka 2021 na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa FIFA mwaka 2022, akiwa amefunga mabao 857.

Lakini Ronaldo ana njaa ya kuvunja rekodi zaidi kabla ya kustaafu soka lake na kukiri ana matumaini ya kutimiza kauli aliyopewa na Rais wa Porto, Jorge Nuno Pinto afikishe mabao 1,000.

“Pinto aliniwekea changamoto ya kufikisha mabao 1,000, Ronaldo alisema kufuatia ushindi wa Ureno dhidi ya Slovakia.

“Itakuwa vigumu sana, lakini nataka kujiona jinsi nilivyo na akili. Ikiwa kimwili, miguu yangu itanitendea kama jinsi ninavyoitendea,” alisema Ronaldo.

Ingawa lengo la mabao 1,000 ni changamoto kubwa, mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or alibaki na imani anaweza kufunga mabao 900.

“Hebu tuone,” Ronaldo aliongeza. “Mpaka nifikishe mabao 1,000 lazima nifikishe 900 kwanza. Naamini nitaifikia. Napenda kufikiria kila wakati juu ya malengo ya muda mfupi. Lengo la mabao 900? Ninajiamini, lakini kwa mabao 1,000 itakuwa ngumu.”

Mapema wiki hii, iliripotiwa kuwa Ronaldo ameiarifu Al-Nassr kwamba anataka kusaini mkataba wa kuendelea kukipiga katika klabu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti